MASHINDANO YA VYUO VYA MAFUNZO YA AMALI KUFANYIKA ZANZIBAR
Mamlaka ya Mafunzo ya Amali imeandaa mashindano ya mpira wa
miguu ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya kesho Jumaatatu Agost 14, 2017 ambapo
yatazinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Amani nje kwa kushirikisha vyuo 12
vilivyopo chini ya mamlaka hiyo.
Akizugumza na Mtandao huu mwenyekiti wa kamati ya mashindano
hayo mwalimu Mkubwa Ibrahim Khamisi amesema kwa kuamini michezo ni ajira ndio
maana wakafanya hivyo na lengo nikupata washiriki kwenye mashindano ya elimu
bila malipo.
“Michezo ni ajira ndo mana tumeanzisha mashindano haya,
tunajua vipaji vipo vingi sana Zanzibar, hivyo tunawaomba wadao wa soka
kujitokeza kuangalia vipaji”. Alisema Mkubwa.
Katika Mashindano hayo ambayo yamejumuisha jumla ya Vyuo 12
ambapo vimepangwa katika Makundi 2 tofauti yani kundi A na B.
Kundi A kuna chuo cha Institute of Business and Social Study,
Zanzibar Commercial Institute, Zanzibar Mosquito Net, Chuo cha Wazazi cha Forodhani
na Chuo cha Mwanakwerekwe wakati kundi B kuna chuo cha Melisha, Mwenge, Stone
Town Youth Center, Microtech, Mkokotoni na Chuo cha Ufundi cha Polisi.
Comments
Post a Comment