JKU WABANWA MBAVU NYUMBANI KWAO NA ZESCO YA ZAMBIA


Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya JKU imelazimishwa sare ya 0-0 nyumbani kwao kwenye uwanja wa Amaan dhidi ya Zesco United kutoka Zambia.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na mashambulizi yakushutukizia dakika tisini za muamuzi JeanClaude Ishimwe kutoka Rwanda hakuna timu iliyoona lango la mweziwe zaidi ya kosa kosa nyingi kwa kila timu.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa timu ya JKU Ali Suleiman Mtuli amesema mchezo ulikuwa nzuri na wanajipanga kwa ajili ya mchezo ujao utakaochezwa huko Zambia.

Nae Haji Juma (Chafu) mlinda mlango wa JKU amefanikiwa kuwa nyota wa mchezo huo na amesema wataendelea kupigana ili waiwakilishe vyema Zanzibar katika Mashindano hayo.

Nae kocha wa timu ya ZESCO United Tenant Chembo amesema ameyapokea matokeo hayo huku wakijipanga kwa mchezo wao wa marejeano nyumbani kwao.

Wawakilishi wengine wa Zanzibar timu ya Zimamoto watarajiwa kujitupa dimbani kesho mnamo majira ya saa kumi alsiri kukipiga na timu ya Wolaitta Dicha kutoka nchini Ethiopia ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho barani Afrika.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS