4 BORA DARAJA LA PILI WILAYA YA MJINI KUANZA APRIL 30, MLANDEGE, KWEREKWE CITY, GULIONI NA AMAN FRESH KUPIGANA


Hatua ya nne bora ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini ambapo wanatafutwa Bingwa na Makamo Bingwa wa Wilaya hiyo watakaowakilisha katika Mabingwa wa Wilaya kupigania nafasi za kupanda daraja la 2 Taifa kwa msimu ujao, ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake April 30, 2017 kati ya timu ya Mlandege dhidi ya Amani Fresh mchezo ambao utapigwa saa 1 ya usiku.

Mchezo mwengine utapigwa Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa ZFA Wilaya ya Mjini Yahya Juma Ali amesema ligi yao itakuwa na ushindani mkubwa kwani timu zote 4 zilizofanikiwa ni ngumu.

“Hii 4 bora ya mwaka huu si mchezo kwa vile timu zote zinaushindani wa hali ya juu”. Alisema Yahya.


Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo Magharibi “A”, Magharibi “B”, Kaskazini “A”, Kaskazini “B”, Kati na Wilaya ya Kusini kwa kucheza ligi ya Mabingwa wa Wilaya ambayo itakuwa na timu 14 huku timu 4 zikitafutwa kupanda Daraja la Pili Taifa Msimu ujao.
Kikosi cha Kwerekwe City
Kikosi cha Gulioni

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS