HAPATOSHI LEO USIKU MLANDEGE V/S AMAN FRESH, KESHO WATOTO WA MOO KWEREKWE CITY V/S GULIONI 4 BORA WILAYA YA MJINI


Hatua ya nne bora ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini ambapo wanatafutwa Bingwa na Makamo Bingwa wa Wilaya hiyo watakaowakilisha katika Mabingwa wa Wilaya kupigania nafasi za kupanda daraja la 2 Taifa kwa msimu ujao, ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo April 30, 2017 kati ya timu ya Mlandege dhidi ya Amani Fresh mchezo ambao utapigwa saa 1 ya usiku.

Mchezo mwengine utapigwa kesho Mei Mosi kati ya Gulion na Kwerekwe City mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Mchezo huo ni wa kulipana kisasi kwani msimu huu timu hizo zilikutana Jumapili ya Disemba 4, 2016 katika hatua ya Makundi ambapo Gulioni alipigwa mabao 5-0 dhidi ya City, sasa sijui kesho itakuaje Gulioni atalipa kisasi au City ataendeleza ubabe.

Bingwa na Makamo Bingwa katika ligi hiyo watawakilisha Wilaya ya Mjini kwenda kucheza na Wilaya nyengine sita zikiwemo Magharibi “A”, Magharibi “B”, Kaskazini “A”, Kaskazini “B”, Kati na Wilaya ya Kusini kwa kucheza ligi ya Mabingwa wa Wilaya ambayo itakuwa na timu 14 huku timu 4 zikitafutwa kupanda Daraja la Pili Taifa Msimu ujao.
Kikosi cha Gulioni

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS