K ocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 23 ambao wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya DR Congo na Algeria. Wachezaji wa tano wa Zanzibar ni mlinda mlango Abdulrahman Mohamed wa JKU, pamoja na viungo Mudathir Yahaya wa Singida United, Feisal Salum wa JKU, Abdulaziz Makame wa Taifa ya Jang’ombe na Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar. Kikosi kamili kilichotangazwa na Mayanga kinajumuisha wachezaji wafuatao: Magolikipa ni Aishi Manula, Abdulrahman Mohamed na Ramadhani Kabwili. Walinzi: Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni na Abdi Banda. Viungo: Hamisi Abdallah, Mudathir Yahaya, Said Ndemla, Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Mohamed Issa, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib. Washambuliaji: Mbwana Samatta, John Bocco, Simon Msuva na Yahaya Zayd. Mara ya mwisho Mayanga alitaja kikosi cha Stars Oktoba 24,...
Baada ya siku ya Alhamis ya Machi 16, 2017 chama cha soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) sasa mambo yanazidi kuwa mazuri kufuatia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania {TFF } kupeleka maombi kwenye Shirikisho la Soka Duniani { FIFA } kuiomea Zanzibar kuwa Mwanachama wa Shirikisho hilo. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Muandamizi anayeshughulikia ruzuku wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania {TFF} Derek Murusuri wakati akiwasilisha salamu za Rais wa Shirikisho hilo Jamal Malinzi kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Baraza la Wawakilishi Mbweni. Derek Murusuri alisema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limeshaiandikia Barua rasmi FIFA kuhusu suala hilo lilalosubiriwa na wapenda soka wa Visiwa vya Zanzibar kuwa na uweo wa kushiriki moja kwa moja michezo ya Kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho hilo la Dunia. Alisema mipango inaandaliwa na Uongozi wa juu wa TFF katika kuhakikisha inaipatia nakala Zanzibar...
Timu za JKU Academy zinaondoka usiku wa leo kwa boti ya usiku kwenda Jijini Dar es salam kisha saa 12 za asubuhi kesho Jumatatu kuanza safari ya Arusha ambapo wanakwenda katika Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati (Rolling Stone) mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi July 9-19, 2017. JKU mwaka huu wanatarajia kushiriki timu tatu tofauti katika Mashindano hayo ikiwemo timu chini ya miaka 13, 15 na 17 ambapo msafara wa watu 60 ukitarajiwa kuondoka Visiwani Zanzibar usiku wa leo. Msafara huo ambao utajumuisha timu tatu tofauti za JKU Academy pamoja na waamuzi wao vijana watano na viongozi watano. Mashindano ya Rolling Stone mwaka huu yanatarajiwa kuanza rasmi July 9 na kumalizika July 19, 2017 ambapo msimu huu kumepangwa vituo tofauti makundi mengine yamepangiwa Arusha, mengine Manyara.
Comments
Post a Comment