DK SHEIN AHIMIZA WAZANZIBAR KUWA NA UZALENDO KWA KUIPENDA ZANZIBAR HEROES, HATA WAKIPENDA KINA ARSENAL LAKINI UZALENDO MUHIMU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein amewataka Wanaanchi wa Jimbo la Uzini kuwa na uzalendo wa kupenda chao na kukithamini kwani mtu chake ambapo amewasisitiza kuipenda timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar “Zanzibar Heroes”.

Dkt. Shein ameyasema hayo asubuhi ya leo huko Dunga Wilaya ya Kati kwenye Ukumbi wa Walimu alipokuwa akiwakabidhi Vifaa vya Michezo timu 46 za soka za Jimbo la Uzini ambao wamepewa vifaa hivyo na Muwakilishi wao Mh Mohd Raza.

Amesema katika uzalendo lazima uanze kukipenda chako huku akiwanasihi Vijana hao kuipenda timu ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes”.

“Katika Uzalendo mtu hukipenda chake kwanza, hebu ipendeni kwanza Zanzibar Heroes timu yenu ya Taifa ya Zanzibar, ipendeni Timu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania “Taifa Stars”, muzipende timu zenu huo ndio uzalendo”. Alisema Dkt Shein.

Hata hivyo Dkt Shein amesisitiza kuwa hajamzuia mtu kupenda klabu za Ulaya lakini mtu asipende sana cha nje akakisahau za kwao.

“Hazuiliwi mtu kupenda timu ya nje ya nchi yetu, anaependa Manchester United, Arsenal, Chelsea,  Liverpool sawa tu, najuwa wapo hao! pendeni vile vile lakini musipende mwisho mkajisahau mkaziponda timu zenu, pendeni zote hizo Barcelona, Real Madrid zote zipendeni lakini bado muwe wazalendo wa timu zenu, zetu ndio bora, mukipenda vya nje sana mutavisahau vyenu”. Alisisitiza Dkt Shein.
Zanzibar Heroes
Rais wa Zanzibar Dkt Shein akiwakabidhi vifaa timu za Jimbo la Uzini

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS