HOMA INAZIDI KUWA KALI LIGI KUU ZENJ YAKARIBIA KUMALIZIKA KUTAFUTA TIMU 8 BORA NA 12 ZAKUSHUKA DARAJA

Mzunguko wa 33 wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja unatarajiwa kuanza rasmi kesho Ijumaa kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan.

Ratiba ya mzunguko wa 33 ligi kuu ya soka Zanzibar kanda ya Unguja hiyo.

Ijumaa 28/4 Taifa vs Chuoni saa 10:00 Amaan.

J/mosi 29/4 Polisi vs Kijichi saa 10:00 Fuoni

J/pili 30/4 Mafunzo vs Miembeni saa 8:00 Amaan
J/pili 30/4 JKU vs Mundu saa 10:00 Amaan

J/nne 02/5 Chwaka vs Zimamoto saa 8:00 Amaan
J/nne 02/5 B/Sailors vs Kimbunga saa 10:00 Amaan
J/nne 02/5 Kilimani C vs J/Boys saa 1:00 usiku.

Jumatano 3/5 KMKM vs Malindi saa 8:00 Amaan.
Jumatano 3/5 Kipanga vs KVZ saa 10:00  Amaan.

Timu 2 kati ya nne zilizojihakikishia kutinga hatua ya 8 bora kutoka kanda ya Unguja ni kinara JKU yenye alama 69, Jang’ombe Boys alama 66 huku Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya tatu na Zimamoto inayokamana nafasi ya nne zote bado hazijajihakikishia kutinga hatua hiyo wakiwa na alama sawa 58 huku Polisi ambayo inakamata nafasi ya tano kwa alama 54 ikiwaombea dua Taifa au Zimamoto kuharibu ili kupata wao nafasi hizo, lakini Taifa na Zimamoto wakishinda mchezo mmoja tu kati ya hiyo miwili iliyobakia wanajihakikishia kutinga 8 bora na Polisi hatoweza kuwafikia hata ashinde michezo yote yake miwili.

Kwa upande wa kanda ya Pemba timu 4 tayari zishajulikanwa zilizotinga 8 bora ambazo ni Jamhuri, Mwenge, Kizimbani na Okapi zote kutoka Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Lakini homa nyengine kali ni upande wa kushuka daraja kanda ya Unguja timu 5 kati ya 6 tayari zimeshajulikanwa za kushuka daraja katika hatua ya awali huku moto mkali upo kwa Malindi ambae nae yupo katika mstari mwekundu akimuombea mabaya Kipanga ambapo Kipanga mpaka sasa ameondoka kwenye mstari huo mwekundu akishika nafasi ya 12 kwa alama 41 huku Malindi ambae yupo kwenye mstari mwekundu nafasi ya 13 ana alama 39 na wote wakiwa wamebakiwa michezo miwili mkononi.

Kikosi cha KVZ
Kikosi cha Kipanga

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS