MECHI ZA MWISHO ZA LIGI KUU ZENJ ZAPELEKEA KUBADILIKA KWA RATIBA ILI KUEPUSHA KUPANGA MATOKEO

Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imebakisha mizunguko miwili ili kumalizika lakini homa kali zaidi ni kila mmoja anataka kujua ni timu gani ambazo zitafanikiwa kucheza 8 bora na timu zipi 6 ambazo zitateremka daraja katika hatua ya awali.

Leo Kamati Tendaji ya ZFA Unguja  imeamua kufanya mabadiliko madogo ya ratiba baada ya kupokea agizo kutoka kwa uongozi wa uwanja wa Amaan sambamba na kuepusha upangaji wa matokeo.

Mabadiliko ambayo yamefanywa yamepelekea siku ya Ijumaa ya April 28, 2017 kuchezwa michezo mitatu ambapo KMKM watasukumana na Malindi saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Amaan ambapo muda huo huo katika Uwanja wa Fuoni watacheza kati ya Kipanga dhidi ya KVZ , na mchezo wa Chuoni dhidi ya Taifa ya Jang’ombe utapigwa saa 1:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan.

Siku ya Jumamosi ya April 29, 2017 utapigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Fuoni saa 10:00 za jioni kati ya Kijichi dhidi ya Polisi.

Mei 4, 2017 kutapigwa michezo miwili saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Fuoni Black Sailors dhidi ya Mundu, na saa 1:00 za usiku katika Uwanja wa Amaan watasukumana kati ya Jang’ombe dhidi ya Mafunzo.

Timu 2 kati ya nne zilizojihakikishia kutinga hatua ya 8 bora kutoka kanda ya Unguja ni kinara JKU yenye alama 69, Jang’ombe Boys alama 66 huku Taifa ya Jang’ombe iliyopo nafasi ya tatu na Zimamoto inayokamana nafasi ya nne zote bado hazijajihakikishia kutinga hatua hiyo wakiwa na alama sawa 58 huku Polisi ambayo inakamata nafasi ya tano kwa alama 54 ikiwaombea dua Taifa au Zimamoto kuharibu ili kupata wao nafasi hizo.

Timu 6 zilizokuwepo kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja ni Malindi, Mundu, Kijichi, Miembeni, Chwaka na Kimbunga ambapo moja tu kati ya hizo ikijikaza na kuomba wajuu wake waharibu inaweza ikanusurika ambayo ni Malindi.
Kikosi cha Black Sailors

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS