BOYS KIDUME MBELE YA TAIFA, KWENYE HISTORIA WAONGOZA KUWAFUNGA WENZAO MARA NYINGI

Timu ya Jang’ombe Boys jana imeweka rikodi njema baada ya kuifunga Taifa ya Jang’ombe bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja ulisukumwa saa 2 za usiku kwenye uwanja wa Amaan.

Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Khamis Mussa (Rais) katika dakika ya 86.

Huu ni mchezo wa 6 kukutana katika historia za timu hizi ambapo katika michezo hiyo waliyokutana Taifa alishinda miwili, na Boys kushinda mitatu na mmoja kutoka sare, hivyo mpaka sasa Boys anarikodi nzuri kuliko Taifa.

RIKODI USO KWA USO BOYS V/S TAIFA

WAMEKUTANA MARA 6 MPAKA SASA
Msimu wa mwaka 2012-2013
Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini Taifa 1-2 Boys
Ligi ya Waamuzi dakika 90 Taifa 0-0 Boys, Penalti Taifa 4-5 Boys.

Novemba 19, 2016
Bonanza la Coconut FM Taifa 2-0 Boys
Mabao yalifungwa na Mkongo Baraka Ushindi na Mkenya Mohd Said “Mess.

Disemba 10, 2016
Ligi kuu soka ya Zanzibar Mzunguko wa kwanza Taifa 2-2 Boys
Mabao ya Taifa siku hiyo alifunga Omar Yussuf Chande dakika 9 na Abdallah Mudhihir (Mido) dakika 60 wakati mabao ya Boys yote alifunga Khamis Mussa (Rais) dakika ya 45 na 53.

Disemba 30, 2016
Kombe la Mapinduzi 2017 Taifa 1-0 Boys
Bao pekee lililofungwa na Hassan Seif “Banda”.

Jana April 25, 2017
Taifa ya Jang’ombe 0-1 Jang’ombe Boys

Bao pekee limefungwa na Khamis Mussa (Rais).
Wachezaji wa Jang'ombe Boys wakishangiria na Mashabiki wao baada ya kumalizika mpira

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS