AFRICAN MAGIC YAWATESA KVZ, KOMBE LA MUUNGANO

Kikosi cha African Magic
Mashindano ya Kombe la Muungano 2017 kwa mpira wa Kikapu (Basketball)  yameendelea tena saa 2 asubuhi ya leo Jumatatu katika Uwanja wa Gmkhana ambapo timu ya African Magic ya Wanawake ikafanikiwa kuwafunga Maafande wa KVZ kwa vikapu 72-31.

Mchezo mwengine umepigwa majira ya saa 4 za asubuhi katika Uwanja huo ambapo walicheza Wanaume timu ya Stone Town dhidi ya Nyuki ambapo Wana Jeshi wa Nyuki wakafanikiwa kushinda kwa vikapu 79-59.

Mechi nyengine za leo zote ni kwa upande wa Wanaume ambapo mchezo unaoendelea sasaivi saa 6 za mchana ni kati ya Polisi dhidi ya JKT, na saa 8 za mchana watakipiga timu ya Mbuyuni dhidi ya Tanado, saa 10 za jioni African Magic dhidi ya Stone Town.


Kombe hilo litaendelea tena kesho Jumanne ya April 24, kwa kupigwa mchezo mmoja tu saa 2 za asubuhi kwa Wanaume wa Tonado kutokea Tanzania bara dhidi ya Chake ya Pemba ambapo watasukumana katika Uwanja wa Gmkhana.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS