ALI MOHAMMED AZIPA TANO TIMU ZA PEMBA ZILIZOTINGA 8 BORA

MAKAMO wa Rais wa ZFA Taifa, Ali Mohamed amezipongeza timu za Pemba ambazo zimeingia katika hatua ya 4 bora na kuzitaka kujiandaa katika
michuano ya Super 8, ambayo inatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.

Akizungumza na viongozi wa timu hizo, huko katika ofisi za ZFA Gombani Chake Chake, Makamo alisema licha ya timu hizo kufanya vizuri katika michezo yao, lakini wana kazi kubwa ambayo imewaelekea.

Alifahamisha kuwa kutokana na kiwango ambacho walikionyesha wakati wakisaka nafasi hiyo, timu hizo zilionekana kiwango chao kiko chini sana, hivyo inatia wasiwasi kwa timu za Pemba hazitoweza kuleta
ushindani kwa timu za Unguja.

“Tumemaliza michezo yetu kwa upande wetu na sasa kilichobakia ni kujiandaa, kushiriki katika hatua ya nane bora ila nilichokiona mimi hakuna timu hata moja, ambayo itaweza kutoa upinzani na timu za Unguja
kwani kiwango chetu kiko chini sana”. Alifahamisha Makamo.

Alifahamisha kuwa kiwango kinachoonyeshwa na timu za Pemba ni dhahiri kuwa kwa mfumo wa 12 bora, ambao utachezwa hapo mwakani hakuna hata timu moja kutoka Kisiwani huko ambayo itaweza kushiriki michuano hiyo.

Akizungumzia suala la nidhamu ndani ya michezo, Makamo huyo alisema kumekuwa na vitendo vingi ambavyo vinahatarisha maisha ya viongozi wa
juu Chama hicho, kwa Pemba pamoja na matusi makali makali kutoka kwa baadhi ya viongozi au wapenzi wa timu.

“Mfano ndugu zangu wa Maji maji ya Tumbe, walikuwa ni timu moja wapo ambayo ilikuwa na ustaraabu wa hali ya juu, lakini kwa sasa imebadilika na kufuata nyayo za wenzake kwa matusi”.

Hata hivyo aliviomba vilabu hivyo kutunza nidhamu na kufuata maadili yaliyo mazuri, pamoja na kuwataka kucheza mpira na kuacha chuki miongoni mwa timu na timu au mtu na mtu kwani hilo halitowafikisha wanakotaka.

Katibu wa Mwenge F.C Gongo Shaaban Gongo, alikitaka Chama hicho kutafuta mbinu mbadala ambazo zitaweza kuondosha tofauti zilizopo katika vilabu vya Pemba.

Alisema ushirikiano kwa vilabu vya pemba, jambo hilo halipo na hivyo umeweza hata kubadilisha viwango kwa wachezaji, hata kushusha hadhi ya
mchezo huo kwa Pemba.

Katibu wa Kizimbani Juma Ali Salim, ameupongeza uongozi wa ZFA kwa kuwajali na kuwataka kushirikiana, katika michuano inayowabili mbele yao kwani wana kazi kubwa.
Ali Mohammed

Hata hivyo vilabu hivyo vimeahidi kujiandaa vya kutosha kuhakikisha, timu nne hizo zinafika mbali hata mara hii kuchukuwa ubingwa au nafasi ya pili, kwa upande wa Pemba ni Jamhuri, Mwenge, Kizimbani na Okapi

zote kutoka mkoa wa kaskazini Pemba.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS