BINGWA WA LIGI KUU ZENJ HAJULIKANI ATAPEWA NINI, CENTRAL WILAYA YA MJINI WATATOA MILIONI 1 KWA BINGWA

Wajumbe wa Kamati ya Central W Mjini wakiwa pamoja na Mkanga (Aliyevaa Shati wa kati)

Kamati ya central Wilaya ya Mjini imekabidhiwa shilingi Milioni tatu kwaajili ya Zawadi kwa washindi 6 wa Mashindano yao ya Ligi na ya Kombe la Mtoano yanayotarajiwa kumailizika Jumamosi ya Mei 12, 2018 asubuhi katika uwanja wa Amaan.

Akiwakabidhi fedha hizo Mkurugenzi wa Kampuni ya Raskazone Trader Ali Khatib Mkanga amewaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia michezo hasa ngazi za chini kwani ndiko vipaji vinakotokea.

Mkanga pia amewapongeza viongozi hao wanaosimamia soka la Vijana ndani ya Wilaya ya Mjini kwa mafanikio yao ya kusimamia vyema Soka hilo la Vijana.

Nae katibu msaidizi wa Kamati ya Central Wilaya ya Mjini Alawi Haidar Foum amempongeza Mkanga kwa kusaidia soka la Vijana huku akiwataka watu wengine wasaidie Michezo hasa Vijana kwani ndio msingi imara wa Maendeleo.

Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa kamati hiyo Ali Suleiman (Kisheta) amesema kamati yao imepanga kuanzisha Kombain kwa kila daraja lao ili kuzidi kutoa ushindani kwa wachezaji kwani Wachezaji watajituma zaidi kuhakikisha wanachaguliwa katika Kombain hizo.

Mashindano ya Central Ligi yatafungwa rasmi 12/05/2018 kwa kupigwa michezo mitatu katika Uwanja wa Amaan kwa kuchezwa fainali tatu za kombe la Mtoano ambapo Daraja la Juvenile (U-14) watacheza kati ya Weles dhidi ya Barcelona, daraja la Junior (U-17) watacheza kati ya New Afrika na Real Kids huku kwa upande wa daraja la Central (U-21) watasukumana kati ya Mapembeani dhidi ya King Boys.

Bingwa wa Mashindano hayo watazawadiwa fedha Taslim Shilingi Milioni moja pamoja na zawadi nyengine ambapo mpaka sasa mabingwa kwa upande wa ligi ni Sevilla (Juvenile), Barcelona (Junior) na Mapembeani (Central) huku wakisubiriwa kwa hamu kubwa mabingwa wengine wa Kombe la Mtoano Jumamosi.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS