KIONGOZI MWENGINE MKUBWA WA ZFA AJIUZULU


Makamo wa Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA PEMBA) Ali Mohammed nae amejiuzulu rasmi nafasi yake kuongoza chama hicho.

Taarifa kama hiyo ni muendelezo ndani ya chama hicho kufutia viongozi wengine wajuu akiwemo akiwemo alokuwa Rais Ravia Idarous Faina pamoja na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali nao kujiuzulu siku chache zilizopita.

Inaonekana wazi chanzo cha viongozi wote hao kujiweka pembeni ni kuhusu uzembe uliofanywa kati yao na kupelekea timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana U-17 (Karume Boys) kuondolewa katika Mashindano ya CECAFA na kupigwa faini ya Dola elfu kumi na tano pamoja na kuzuiliwa kutoshiriki Mashindano yote yatakayoendeshwa na Baraza hilo mpaka kulipa kwa faini hiyo kwa kosa la kupeleka wachezaji wakubwa waliozaliwa chini ya tarehe 01/01/2002.

ZFA ilizungumza na Vyombo vya Habari kupitia Makamo wake huyo (Ali Mohammed) na kukataa kuwa CECAFA hawajatuma ufafanuzi wa umri kwa wachezaji walotakiwa kushiriki mashindano ya CECAFA ya Vijana (U-17) yalofanyika Burundi mwaka huu huku ikimtupia lawama katibu wa CECAFA Nicholas Musonye.

Lakini mapema mwezi uliopita alokuwa Makamo wa Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali alikiri kupokea barua inayofafanua kuhusu umri wa wachezaji wanaotakiwa kushiriki katika mashindano hayo jambo ambalo likionekana yeye ndio nambari moja wa kulaumiwa mpaka mwenyewe akaamua kujiuzulu.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS