MSHAMBULIAJI WA SERENGETI BOYS AIKOA TIMU YA MJINI UNGUJA
![]() |
Mkoko alipokuwa Gentil, Gabon AFCON U-17 |
Mshambuliaji wa Klabu ya Miembeni City, Ibrahim Abdallah “Imu
Mkoko” jana aliikoa timu yake ya Kombain ya Mjini Unguja baada ya kufunga bao
la kusawasisha katika dakika ya 69 na kufanya matokeo kuwa 2-2 dhidi ya Dulla
Boys katika mchezo wa kirafiki uliopigwa majira ya saa 3 usiku katika Uwanja wa
Amaan.
Katika mchezo huo Mjini ndio wa mwanzo kupata bao katika
dakika ya 24 kupitia Yakoub Amour kisha Dulla Boys wakajibu mapigo katika
dakika ya 33 kupitia Ali Haji na kwenda mbele 2-1 katika dakika ya 44 baada ya
Simai Ali kufunga bao hilo la pili ndipo dakika ya 69 Mkoko akaikoa timu yake
na kuufanya mchezo umalizike 2-2.
Mkoko alijumuishwa katika kombain hiyo punde tu aliporejea
Visiwani Zanzibar mwezi uliopita akitokea mjini Gentil, Gabon katika michuano
ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya AFCON akiitumikia timu ya Taifa ya
Tanzania “Serengeti Boys” baada ya kutolewa kwa kufungwa 1-0 na Niger katika
mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil, nchini Gabon.
Tayari Mkoko, amekuwa tegemeo katika kikosi cha timu hiyo na
wamekuwa wakimtumia kuwa mshambuliaji wa kati tegemeo na wenyewe Mjini Unguja
wanatarajia kufanya vyema kwenye Mashindano ya Vijana ya Rolling Stone ambayo
yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake kuanzia June 29, 2017 na kumalizika July
9, 2017 huko Mbulu, Manyara.
Comments
Post a Comment