Mlinzi wa kati wa timu ya Yanga Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ sasa atavaa jezi nambari 23 iliyokuwa ikivaliwa na aliyekuwa Nahodha wa timu, Nadir Haroub 'Cannavaro'ambae amestaafu rasmi soka la ushindani. Ninja ambae siku moja alitamani kucheza pamoja na Cannavaro kisha pia kutamani baada ya kustaafu nyota huyo jezi yake nambari 23 kuirithi yeye ndoto hizo zimetimia baada ya kukabidhiwa rasmi jezi hiyo badala ya ile 6 aliyovaa msimu uliopita. Jezi ya Ninja ya msimu uliopita (6) sasa itavaliwa na Mzanzibar mwenzake Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyehamia Jangwani kwa kishindo msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar. ‘’ Nimefurahi kuvaa jezi hii mana ilikuwa pia ni ndoto zangu, Cannavaro nilikuwa namuiga sana style yake tangu nikiwa mdogo na yeye ananishauri mambo mingi na kunipa moyo ntajitahidi namimi kufanya kazi na Mungu atanisaidia kuisadia timu yangu ya Yanga’’. Alisema Ninja. Wakati huo huo baada ya aliyekuwa Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kustaaf...