MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KUSHUHUDIA RESI ZA BAISKELI

MASHINDANO ya mbio za baiskeli North Zanzibar Sportive mwaka huu yatafanyika Agosti 19, Visiwani Zanzibar ambazo zitaanza na kumalizika Nungwi Kazkazini mwa Kisiwa cha Unguja na zaidi ya washiriki 200 watakimbia Kilometa 50 na 100 kwa wanaume na wanawake.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ikuhusiana na matayarisho hayo  Mkurugenzi wa Mbio hizo Abrahman Hussein amesema lengo la kuanzisha mashindano ni kuibua vipaji vya wakimbiaji wa mbio za Baskeli pamoja na kuisaidia Jamii ambapo wamepanga kusaidia ujenzi wa Skuli ya Chekechea ya Nungwi.

Amesema mashindano hayo yatasaidia kuongeza idadi ya Watalii nchini na kuongeza pato la taifa na wananchi mmoja mmoja pamoja na ongeza la ajira kwa vijana.

Nao baadhi ya Wadhamini wa Mashindano hayo wamesema wameamua kusaidia Mashindano hayo kwa kumfata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein ambae analengo la kurejesha vugu vugu la Michezo Zanzibar.

Kwa upande wake msemaji wa chama cha Baskeli Zanzibar (CHABAZA) Saleh Kijiba amesema mashindano hayo yamejumuisha wachezaji wa Zanzibar nzima kwani wapo wengine watakaotoka Kisiwani Pemba kushiriki Mashindano hayo.

Nao baadhi ya waendeshaji baskeli katika Mashindano hayo wamesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda huku wakiwashukuru wadhamini waliojitokeza kudhamini mbio hizo.

Katika Mashindano hayo ambayo yataanzia Nungwi, watapita Kiwengwa, Pwani Mchangani mpaka Pongwe kisha kurejea tena Nungwi walipoanzia ambapo washiriki wote watapatiwa zawadi ya Medali , huku mshindi wa kwanza atapatiwa Shilingi Milioni 1, nafasi ya pili Laki 5 na watatu Laki 3 kwa Wanaume na Wanawake.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS