NINJA RASMI APEWA JEZI YA CANNAVARO YANGA, FEI TOTO NAE ACHUKUA YA MZANZIBAR MWENZAKE

Mlinzi wa kati wa timu ya Yanga Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ sasa atavaa jezi nambari 23 iliyokuwa ikivaliwa na aliyekuwa Nahodha wa timu, Nadir Haroub 'Cannavaro'ambae amestaafu rasmi soka la ushindani.

Ninja ambae siku moja alitamani kucheza pamoja na Cannavaro kisha pia kutamani baada ya kustaafu nyota huyo jezi yake nambari 23 kuirithi yeye ndoto hizo zimetimia baada ya kukabidhiwa rasmi jezi hiyo badala ya ile 6 aliyovaa msimu uliopita.

Jezi ya Ninja ya msimu uliopita (6) sasa itavaliwa na Mzanzibar mwenzake Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyehamia Jangwani kwa kishindo msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar.
‘’ Nimefurahi kuvaa jezi hii mana ilikuwa pia ni ndoto zangu, Cannavaro nilikuwa namuiga sana style yake tangu nikiwa mdogo na yeye ananishauri mambo mingi na kunipa moyo ntajitahidi namimi kufanya kazi  na Mungu atanisaidia kuisadia timu yangu ya Yanga’’. Alisema Ninja.


Wakati huo huo baada ya aliyekuwa Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' kustaafu rasmi soka la ushindani, uongozi wa klabu hiyo umemtangaza Kelvin Yondani kuwa mbdala wake.

Yondani amechukua rasmi kitambaa cha unahodha ndani ya kikosi cha Yanga ambacho alikuwa akikikivaa kama msaidizi ukiachana na Cannavaro ambaye alikuwa Nahodha mkuu.


Kutoka na kustaafu kwa Cannavaro, uongozi Yanga umekabidhi rasmi Yondani kitambaa cha unahodha huo huku atakuwa akisaidiwa na kiungo, Thaban Kamusoko pamoja na beki, Juma Abdul.


Kikosi hicho kipo mjini Morogoro hivi sasa kikijiandaa na mchezo dhidi ya USM Alger na msimu mpya wa ligi unaotarajia kuanza Agosti 22 mwaka huu.


Yanga waliwasili Morogoro jana kwa kambi maalum ya wiki mbili kujiandaa na mchezo dhidi ya Waarabu hao ambao ni wa Kombe la Shirikisho Afrika pia kuelekea Ligi Kuu Bara.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS