4 BORA KUSAKA TIMU 2 KUPANDA LIGI KUU ZENJ MSIMU UJAO KUANZA LEO
![]() |
Wachezaji wa Miembeni City |
Hatua ya nne bora ligi Daraja la Kwanza Taifa kituo cha
Unguja kutafuta timu 2 za kwenda ligi kuu Zanzibar Msimu ujao inatarajiwa
kupigwa Leo Jumatatu April 17 michezo miwili katika Uwanja wa Amaan.
Saa 10:00 za Jioni Ngome waatanza kazi kucheza na Seblen
United huku mchezo mwengine kupigwa saa 1:00 za usiku kati ya Miembeni City
dhidi ya Charawe.
Michezo mengine itapigwa siku ya Jumatano ya April 26 ambapo saa 10:00 za jioni wataumana
kati ya Miembeni City dhidi ya Seblen United, na saa 1:00 za usiku Charawe vs
Ngome.
Michezo ya mwisho itapigwa Mei 9, 2017 ambapo saa 10:00 za
jioni kumi watasukumana Sebleni United dhidi ya Charawe na saa 1:00 za usiku
Miembeni City watamalizana na Ngome michezo yote itachezwa katika uwanja wa Amani
mjini Unguja.
Comments
Post a Comment