CHANEZA CHAAMINI VILABU VYAKE VITAREJEA NA VIKOMBE KENYA
Chama cha Netball Zanzibar (CHANEZA) kipo mbioni kukamilisha
matayarisho ya mwisho ya Safari kwa vilabu vyake ambavyo vinatarajiwa kwenda
Nairobi Nchini Kenya kwenye mashindano ya Klabu bingwa ya Afrika Mashariki ya
Netball ambayo yanatarajiwa kuanza April 23-30 mwaka 2017.
Akizungumza na Mtandao huu Katibu wa CHANEZA Said Ali Mansabu
amesema Mashindano ya msimu huu yatakuwa na ushindani sana lakini kwa upande
wao Zanzibar wamejiandaa vyema kurejea na Vikombe ambapo timu 4 za Zanzibar
zikitarajiwa kuwakilisha nchi.
“Mashindano magumu msimu huu lakini sisi Zanzibar tunategemea
kupeleka timu 4, na pia naamini tutarejea na vikombe”. Alisema Mansabu.
Vilabu vya Zanzibar vitakavyoshiriki Mashindano hayo ni KVZ,
Zimamoto na Mafunzo kwa Wanawake wakati kwa Wanaume watawakilisha JKU pekee.
Comments
Post a Comment