CHWAKA AONA MWEZI, CHUONI HOI KWA KIPANGA
Timu ya Chwaka Stars imefanikiwa kuonja ladha ya Ushindi baada ya kuifumua Kimbunga mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu sika ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa katika uwanja wa Amaan Saa8 za mchana.
Mabao ya Chwaka yamefungwa na Juma Said dakika ya 4, Hafidh Ramadhan dakika ya 5, Ibrahim Sultan dakika ya 26 na Maombi Zabron dakika ya 89.
Mchezo mwengine uliopigwa saa 10 za jioni timu ya Kipanga walifanikiwa kuifunga Chuoni mabao 2-0.
Mabao ya Kipanga yamefungwa na Muughar Ahmada Jihad dakika ya 65 na David Nyerere dakika ya 89.
Kesho ligi hiyo itaendelea tena katika uwanja wa Amaan saa 8 mchana Polisi dhidi ya Mundu na saa 10 za jioni Kilimani City dhidi ya Kijichi.
![]() |
Kikosi cha Chwaka Stars |
Comments
Post a Comment