HAKUNA KUKUSANYA MICHANGO TAIFA, PESA HAZITUFIKII -ASEMA KATIBU WA TAIFA

Uongozi wa Timu ya Taifa ya Jang'ombe umepiga marufuku michango inayochangishwa mitaani kupitia sahani na mabakuli mbali mbali ambapo michango hiyo haifiki kwenye timu husika na mwisho wake wanaochangisha huzichukua na kuzitumia wao binafsi.

Katibu wa Taifa ya Jangombe Mohd Maulid amewataka wadau wa Taifa kusitisha michango yao kwa kuchangia sehemu kama hizo kwani haziwafiki wao kwenye klabu.

Amesema sehemu moja tu ndipo michango yao inawafika ambapo ni Jang'ombe kwa lofi lakini vituo vyengine vyote michango hiyo inatumiwa vibaya kwa wale wanaokusanya.

Timu ya Taifa ya Jang'ombe ni miongoni mwa timu zenye Mashabiki wengi katika soka la Zanzibar ambapo siku hizi kuna watu wengi huchangisha kwa kurandisha Sahani na Mabakuli ili timu hiyo ichangiwe lakini kumbe fedha hizo hazifiki sehemu husika.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE