KARANI WA ZFA AKATWA MGUU KWA MARADHI YA SUKARI
![]() |
Viongozi wa ZFA walipokwenda kumuangalia Karani wao katika Hospitali ya Mnazi Mmmoja |
Karani wa Chama chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Haji
Othman (Babu Haji) amekatwa mguu jana
kwa maradhi ya Sukari baada ya kuwa na vidonda mguuni mwake.
Taarifa tulizozipata kutoka kwa Mjumbe mmoja wa ZFA amesema
Karani wao huyo bado yupo katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmmoja Mjini Unguja.
Alisema sababu kubwa ya kufanyiwa uperesheni huo ni baada ya
kuwa na vidonda vya mguu huo na
kuonekana vingezidi kumletea matatizo
makubwa mwilini mwake ambapo Madaktari wakalazimika kumkata Mguu huo.
“Ni kweli Karani wetu amekatwa mguu na tumuombee dua kwani
ndio mitihani yetu ya Maisha, Mungu atamsaidia”. Alisema mjumbe huyo.
Mwenyezi Mungu atazidi kumsaidia mgonjwa huyo na kumpa subra katika kipindi hiki kigumu.
![]() | |||||||
Makamo Urais wa ZFA Unguja Mzee Zam Ali akimliwaza Babu Haji |
AclibinFfos_ne-Washington Curtis Bethea https://wakelet.com/wake/cmJi74rGrmySBs_PiTXFG
ReplyDeletescisoggata