KOMBE LA MUUNGANO KUANZA KESHO IJUMAA KWA KUSHIRIKISHA VILABU VYA BARA NA ZANZIBAR
![]() |
Kikosi cha Mafunzo |
Mashindano ya Muungano ya Mchezo wa Mpira wa Kikapu
(Basketball) yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya kesho Ijumaa ya April 21 na
kumalizika Jumatano April 26, 2017 kwenye uwanja wa Gymkhana ambapo Mgeni Rasmi
anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.
Akizungumza na Mtandao huu katibu wa chama cha Basketball
Zanzibar (BAZA) Abdul-rahman Mohd Hassan
amesema wamejiandaa vizuri msimu huu na watahakikisha mashindano hayo yatakuwa
bora kuliko miaka iliyopita.
“Mashindano ya mwaka huu tunatarajia kuwa bora zaidi, vilabu
vimepania kufanya makubwa msimu huu, mgeni Rasmi atakuwa Balozi Seif”. Alisema Abdul-rahman.
Kawaida ya Mashindano hayo hujumuisha vilabu vya juu kwenye
ligi kuu ya Basketball ya Tanzania bara na vinne vya juu kwenye ligi ya
Zanzibar ambapo ufunguzi watacheza Polisi dhidi ya Mbuyuni saa 10:00 za jioni.
Kwa upande wa Wanaume mpaka sasa timu zilizothibitisha
kushiriki ni Polisi, Mbuyuni, Nyuki, African Magic, stone town zote za Unguja
pamoja na Tonado ya Kisiwani Pemba wakati kwa Tanzania JKT na timu ya Oilers
ndizo zilizothibitisha mpaka sasa.
Comments
Post a Comment