KWEREKWE CITY YATESA
Ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini hatua ya 8 Bora imeendelea tena leo saa 1 usiku katika Uwanja wa Amaan ambapo Kwerekwe City imefanikiwa kushinda bao 1-0 dhidi ya Aman Fresh.
Bao pekee la City limefungwa na Abdul nassir Gamal dakika ya 89.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja saa 1 katika uwanja wa Amaan kati ya Medson dhidi ya Muembe ladu.
Kwenye kundi hilo Kwerekwe city anaongoza akiwa na alama 6 kwa michezo 2, huku Amani Fresh akiwa na alama 3 michezo 2 wakati Muembe ladu akishika nafasi ya 3 akiwa hana alama hata moja baada ya kucheza mchezo mmoja huku Medson akiburura mkia akiwa hana alama hata moja baada ya kucheza mchezo mmoja.
![]() |
Kikosi cha Kwerekwe City |
Comments
Post a Comment