MAXMILIANA WA TAEKWON-DO AWAPA TANO WAANDISHI WA HABARI
![]() |
Wachezaji wa mchezo wa Taekwon-do |
Kocha mkuu wa mchezo wa Taekwon-do Zanzibar
Maxmiliana Kailangana ametoa shukrani zake za dhati kwa Waandishi wa Habari
baada kuusambaza mchezo huo na kuanza kujulikanwa katika Visiwa vya Zanzibar.
Maxmiliana amesema kwasasa wana zaidi
ya Wachezaji 15 wapya ambao wamevutiwa kujiunga na mchezo huo huku akisisitiza
bila ya Vyombo vya Habari mchezo huo usengejulikanwa.
“Tunawashukuru Waandishi wa Habari
wote ambao wamekuwa nasisi tangu tunaanzisha mchezo huo hapa Visiwani,
maendeleo kwasasa ni mazuri kwani idadi ya wachezaji imezidi na sasa tumewapata
zaidi ya wachezaji 15 wapya ambao wamevutiwa na mchezo huu”. Alisema Maxmiliana.
Taekwon-do ni mchezo mpya kwa
Zanzibar ambapo asili yake ni nchini Korea kwa lugha nyepesi unaweza ukauwita
sanaa ya mapambano ambapo wenzetu Tanzania bara mchezo huu si mgeni lakini
katika Visiwa hivi ndo kwanza unaanza kuanzishwa na kusambazwa kwani wengi
wanaufananisha na mchezo wa karati lakini ni tofauti kabisa licha ya kuwa
mchezo huo pia wanatumia kupiga mateke na kurusha ngumi .
Mchezo huo unafundishwa katika ukumbi
wa Judo Amani Mjini Zanzibar na Kocha Maxmiliana Kailangana ambae katokea
Tanzania bara sasa yupo hapa Zanzibar kuusambaza mchezo huo kwa kila siku ya
Jumatatu, Jumatano na Alhamis kuanzia saa 1:00 usiku hadi 3:00 usiku.
Comments
Post a Comment