MFAUME APATA SHAVU KUCHEZESHA MECHI YA KIMATAIFA
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Mfaume Ali
Nassor wa Zanzibar kuwa mwamuzi wa kati katika mchezo wa Kimataifa wa kugombea
CHAN utakaozikutanisha timu za taifa za Sudani ya Kusini dhidi ya Somalia
utakaofanyika April 22, 2017 huko Djibouti na umelazimika kuchezwa huko kwa
vile wenyeji Somalia nchini kwao bado hakujatulia.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF iliyofika Chama cha Soka
Zanzibar (ZFA) mapema wiki hii, pia imewataja waamuzi wasaidizi ambao wanatoka
Tanzania bara.
Waamuzi hao ambao ni washika vibendera ni Ferdinand Chacha,
Frank Komba wakati mezani atakuwa Israel Nkongo huku Kamishna wa mchezo huo
atatoka Kenya ambaye anaitwa Edil Likono.
Hongera Mfaume nenda kaiwakilishe Zanzibar
ReplyDelete