MFUMO GANI WA KUPATIKANA TIMU 12 ZA MSIMU UJAO, MKUTANO MKUU WA ZFA UTAKAOFANYIKA JUMAMOSI PEMBA UTAJADILI
Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA TAIFA unatarajiwa kufanyika
Siku ya Jumamosi ya April 22, 2017 katika Ukumbi wa Uwanja wa Gombani Kisiwani
Pemba kuanzia saa 3:00 za asubuhi.
Katika Mkutano huo zitajadiliwa Ajenda 5 na mengineyo kati ya
hizo ajenda ikiwemo kuhusu maboresho ya Katiba ya ZFA kuendana na matakwa ya
Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” ambapo hivi karibuni Zanzibar imekuwa
mwanachama wa 55 wa Shirikisho hilo.
Mbali na ajenda hiyo, pia ajenda kubwa zaidi inayosubiriwa
kwa hamu kubwa sana na wadau wa soka Zanzibar ni ajenda nambari 4 kuhusu mfumo
gani utatumika kuzipata timu 12 ambazo zitashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar
kwa msimu ujao wa mwaka 2017 -2018 ambapo kwa msimu huu ligi hiyo ina jumla ya
vilabu 36 kwa kanda zote za Unguja na Pemba, ambapo katika Ajenda hiyo Umoja wa
vilabu watatoa pendekezo kuhusu upatikanaji wa timu 12 za premier.
Ajenda zitakazojadiliwa hizo:-
1. Kupokea taarifa
kuhusu uanachama kamili wa zfa kutoka CAF.
2. Kupokea taarifa
ya mjumbe wa kamati tendaji kutoka wilaya ya Kaskazini “A” na mjumbe kutoka
wilaya ya Mjini.
3. Kupokea taarifa
ya uteuzi wa Mkurugenzi wa ufundi (Technical director).
4. Kupokea pendekezo
kutoka umoja wa vilabu kuhusu upatikanaji wa timu 12 za premier.
5. Kuunda kamati
ndogo ya watu wasiozidi 3 ambao wataifanyia marekebisho katiba ya zfa kwa ajili
ya kwenda sambamba na matakwa ya fifa na caf kwa mujibu wa mazingira ya Zanzibar.
6. mengineyo.
Wajumbe Kutoka Kisiwani Unguja wanatarajiwa kuondoka kesho
kutwa Ijumaa kwa wale ambao watatumia njia ya Bahari na wale wajumbe wengine
watakaotumia njia ya anga wataondoka siku hiyo hiyo ya Jumamosi asubuhi.
Comments
Post a Comment