MIEMBENI CITY NA NGOME ZAANZA VYEMA MBIO ZA KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO

Timu za Miembeni City na Ngome zimefanikiwa kuanza vyema harakati zao za kupanda ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ujao wa mwaka 2017-2018 baada ya kushinda michezo yao ya mwanzo.

City wamepata ushindi wa mabao 2-0 walipoichapa Charawe mchezo uliopigwa saa 1 za usiku leo katika uwanja wa Amaan.

Katika mtanange huo ambao ulikuwa na ushindani kwa pande zote City wamejipatia magoli yao kupitia Seif Salum "Zola" na Muhamed Vuai "Prince".

Mapema saa 10 za jioni leo katika Uwanja wa Amaan Ngome walifanikiwa kuichapa Sebleni United mabao 2-1.

Michezo mengine itapigwa siku ya Jumatano ya  April 26 ambapo saa 10:00 za jioni wataumana kati ya Miembeni City dhidi ya Seblen United, na saa 1:00 za usiku Charawe vs Ngome.

Michezo ya mwisho itapigwa Mei 9, 2017 ambapo saa 10:00 za jioni kumi watasukumana Sebleni United dhidi ya Charawe na saa 1:00 za usiku Miembeni City watamalizana na Ngome michezo yote itachezwa katika uwanja wa Amani mjini Unguja.


Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE