MKUTANO WA ZFA UMESHAANZA KUIBUA MAPYA

Viongozi wa wakuu wa ZFA wakiomba dua ya kuanza mkutano Mkuu



Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA TAIFA unaendelea sasaivi hapa Kisiwani Pemba  katika Ukumbi wa Uwanja wa Gombani  tangu  3:00 za asubuhi.

Katika Mkutano huu  zinajadiliwa Ajenda 5 na mengineyo kati ya hizo ajenda ikiwemo kuhusu maboresho ya katiba ya ZFA kuendana na matakwa ya Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” ambapo hivi karibuni Zanzibar imekuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho hilo.

Mbali na ajenda hiyo, pia ajenda kubwa zaidi inayosubiriwa kwa hamu kubwa sana na wadau wa soka Zanzibar ni ajenda nambari 4 kuhusu mfumo gani utatumika kuzipata timu 12 ambazo zitashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu ujao wa mwaka 2017 -2018 ambapo kwa msimu huu ligi hiyo ina jumla ya vilabu 36 kwa kanda zote za Unguja na Pemba, ambapo katika Ajenda hiyo Umoja wa vilabu watatoa pendekezo kuhusu upatikanaji wa timu 12 za premier.

Ajenda ambazo zinajadiliwa hizo:-
1.      Kupokea taarifa kuhusu uanachama kamili wa zfa kutoka CAF.
2.      Kupokea taarifa ya mjumbe wa kamati tendaji kutoka wilaya ya Kaskazini “A” na mjumbe kutoka wilaya ya Mjini.
3.      Kupokea taarifa ya uteuzi wa Mkurugenzi wa ufundi (Technical director).
4.      Kupokea pendekezo kutoka umoja wa vilabu kuhusu upatikanaji wa timu 12 za premier.
5.      Kuunda kamati ndogo ya watu wasiozidi 3 ambao wataifanyia marekebisho katiba ya zfa kwa ajili ya kwenda sambamba na matakwa ya fifa na caf kwa mujibu wa mazingira ya Zanzibar.
6.      mengineyo.

Katika mkutano huo kuna baadhi ya Wajumbe wanatarajiwa kufukuzwa katika Chama hicho, zaidi endelea kufatilia Blog hii.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu ZFA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS