SAILORS NA JKU NGUVU SAWA, KVZ NA TAIFA WASHINDA

Mzunguko wa 31 wa ligi kuu Zanzibar kanda ya Unguja leo hii umeanza kuchukuwa nafasi yake kwenye dimba la Aman ambapo majira ya saa 8 Jku wakashindwa kutamba mbele ya Black Sailors baada ya kulazimishwa sare isio na magoli.

Saa 10 za jioni KVZ ikatoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Malindi,  bao pekee likifungwa na Mohd Nasor dakika ya 87 pia katika mchezo huo mchezaji Mohd Iddi wa Malindi alitolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu.

Saa 1 Usiku Miembeni wakakubali kufungwa 2-0 na Taifa ya Jang'ombe.
Mabao ya Taifa yakifungwa na Mkenya Mohd Said "Mess" na Mkongo Meta Apping.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho saa 8:00 za mchana Chwaka vs Kimbunga na saa 10:00 za jioni Chuoni vs Kipanga.

Kikosi cha Black Sailors

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE