SQUASH KUMEKUCHA UCHAGUZI MEI
Chama cha Mpira wa Ukuta Zanzibar “Zanzibar Squash Racket Association (ZSRA)” kipo mbioni kufanya Uchaguzi wake ambao
unatarajiwa kufanyika Mei 6, 2017 ambapo mpaka sasa haujajulikanwa utafanyika
katika ukumbi gani.
Zoezi hilo litaanza harakati zake kuanzia April 17-19, 2017
ambapo fomu zitaanza kuchukuliwa kwenye Uwanja wa Squach uliopo Polisi Ziwani
Mjini Unguja ambapo April 23, 2017 ndio mwisho wa kurejesha fomu wakati huo huo
April 24 ni siku ya kutajwa majina ya Wagombea ambapo April 25 ni siku ya
kupokea malalamiko na pingamizi ambapo April 26 ni siku ya kusikilizwa
pingamizi, baada ya hapo April 27-28 watahojiwa wagombea na kamati hiyo na Mei
5, 2017 ni siku ya mwisho ya kupiga kampeni ambazo zitaanza tangu April 24.
Uchaguzi huo ambao utagombewa nafasi 6 zikiwemo Mwenyekiti,
Makamo Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mshika Fedha na Mshika Fedha
Msaidizi.
Kamati itakayosimamia Uchaguzi huo ina wajumbe 7 wakiongozwa
na Mwenyekiti Abdallah Juma na Katibu Yussuf Mohd Ali “Kareka” huku wajumbe
wakiwa Juma Mussa Rashid, Omar Makungu Omar, Mwanaidi Abdallah Makame, Zuhura
Mohd Ali na Hadia Yahya Khamis.
Kamati hiyo imeweka hadharani sifa 6 za kuwa mgombea .
1.
Mgombea
asipungue miaka 30.
2.
Mgombea
awe amemaliza kidato kuanzia cha pili (Form II).
3.
Mgombea
awe Mzanzibar.
4.
Mgombea
awe hajawahi kufungwa.
5.
Mgombea
awe ni mpenzi wa mchezo wa Squach.
6.
Mgombea
awe na akili timamu.
Kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho kila baada ya miaka 4
hufanyika Uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya ambapo Uchaguzi uliopita
ulifanyika mwaka 2012.
Comments
Post a Comment