TIMU 12 ZA LIGI KUU MSIMU UJAO KUPATIKANA BAADA YA KUMALIZIKA 8 BORA NDIPO VILABU 28 KUPANGA KWA PAMOJA
![]() |
Viongozi wakuu wa ZFA |
Wadau wengi wa soka Visiwani Zanzibar wanahamu sana kujua
mfumo gani utatumika kwaajili ya kupatikana timu 12 za ligi kuu soka ya
Zanzibar kwa msimu ujao wa mwaka 2017-2018.
Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA uliokaa asubuhi ya leo kwenye
Ukumbi wa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba umependekeza vilabu 28 vya ligi kuu
ya Zanzibar msimu huu wakutane kwa pamoja baada ya kumalizika 8 bora na kupanga
ni mfumo gani utumike ili zipatikane timu 12 za msimu ujao.
Timu hizo 28 ni zile ambazo zitanusurika kushuka daraja
katika mkumbo wa awali ambapo hushuka timu 12 kwa kila kanda hushuka 6, yani
Unguja 6 na Pemba.
Viongozi wa timu hizo 28 za Unguja na Pemba watakutana kwa
pamoja baada ya kumalizika hatua ya 8 bora ambapo hapo ndipo patakapojulikanwa
timu zipi zitacheza ligi kuu msimu ujao.
Hivyo pengine huwenda timu ikafanikiwa kuwa bingwa au Mshindi
wa Pili wa Zanzibar (Wawakilishi wa Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho) lakini
akashindwa kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu ujao endapo akishindwa kuvuka
katika mfumo huo ambao utakaotumika.
Msimu huu wa mwaka 2016-2017 ligi kuu soka ya Zanzibar ina
jumla ya timu 36 zikijumuisha 18 za Unguja na 18 za Pemba lakini ZFA baada ya
kuwa mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Afrika “CAF”, Shirikisho hilo
limekitaka chama hicho kuwa na vilabu 12 kwa msimu ujao wa mwaka 2017-2018.
Comments
Post a Comment