8 BORA KUANZA KESHO ZIMAMOTO NA JKU, JUMAPILI BOYS NA TAIFA
![]() |
Kikosi cha Zimamoto |
Hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar inatarajiwa
kuanza kesho Jumamosi ya Mei 13, 2017 kwa kupigwa michezo miwili katika Viwanja
viwili tofauti.
Katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba wataanza Kizimbani
dhidi ya Okapi saa 10 za jioni ambapo Kisiwani Unguja katika Uwanja wa Amaan
watasukumana JKU dhidi ya Zimamoto saa10:00 za jioni.
Jumapili ya Mei 14 itaendelea tena kwa kupigwa mchezo kati ya
Mwenge dhidi ya Jamhuri saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Gombani huku Amani
Mjini Unguja kutakuwa na homa ya Jiji la Jang’ombe kati ya Taifa ya Jang’ombe
dhidi ya Boys saa 2:00 za usiku.
RATIBA KAMILI MZUNGUKO WA KWANZA
Jumamosi 13/5/2017 Kizimbani v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
Jumamosi 13/5/2017 JKU v/s Zimamoto, saa 10:00 Amaan.
Jumapili 14/5/2017 Mwenge v/s Jamhuri, saa 10:00 Gombani.
Jumapili14/5/2017 Taifa ya Jang’ombe v/s Jang’ombe Boys, saa 2:00 usiku Amaan.
MZUNGUKO WA PILI
Jumatano 17/5/2017 Zimamoto v/s Jang’ombe Boys, saa 10:00 Amani.
Jumatano 17/5/2017 Kizimbani v/s Mwenge, saa 10:00 Gombani.
Alhamis 18/5/2017 Taifa ya Jang’ombe v/s JKU, saa 10:00 Amaan.
Alhamis 18/5/2017 Jamhuri v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
MZUNGUKO WA TATU
Jumapili 21/5/2017 Jang’ombe Boys v/s JKU, saa 10:00 Amaan.
Jumapili 21/5/2017 Mwenge v/s Okapi, saa 10:00 Gombani.
Jumatatu 22/5/2017 Zimamoto v/s Taifa Jang’ombe, saa 10:00 Amaan.
Jumatatu 22/5/2017 Jamhuri v/s Kizimbani, saa 10:00 Gombani.
Baada ya hapo ligi hiyo itasimama na kupisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo itakuja kuendelea Mzunguko wa nne mpaka imalizike Mwezi huo wa Ramadhan.
|
Comments
Post a Comment