BAZA KUMEKUCHA WAJIPANGA KUFANYA UCHAGUZI JUNE, WATAKA KUTEKELEZA AGIZO LA BTMZ

Kikosi cha Mafunzo cha Basket ball

Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar  “BAZA” kipo mbioni kufanya Uchaguzi wake ambao unatarajiwa kufanyika Mwezi wa June, 2017 ambapo mpaka sasa haujajulikanwa utafanyika tarehe gani.

Akizungumza na Mtandao huu wa kisanduzenj.blogspot.com makamo mwenyekiti wa BAZA Rashid Hamza amesema kwasasa wapo katika harakati za kufanya uchaguzi wao ambao utafanyika mwishoni mwa mwezi wa June mwaka huu.

“Sasa tupo mbioni kufanya uchaguzi, na uchaguzi wetu tunatarajia kufanya ndani ya mwezi wa sita, kwasasa tunaendelea na mchakato huo na mambo yanakwenda vizuri mpaka muda huu”. Alisema Hamza.

Hivi karibuni BARAZA la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), limeviagiza vyama vya michezo  ambavyo havijafanya uchaguzi  kufanya hivyo ili kupata viongozi kulingana na katiba zao ili waongoze kwa demokrasia na kwa kufuata katiba.

Vyama vitano (5) ambavyo vinaharakishwa kufanya uchaguzi ndani ya mwezi June, 2017 ni Chama cha Basketball Zanzibar (BAZA), Chama cha Baskeli Zanzibar (CHABAZA), Chama cha Mpira wa Netball Zanzibar (CHANEZA), Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar yani Hand ball na Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar yani Table Tennis.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS