BENDERA YA CAF YAENDELEA KUPEPEA KATIKA UWANJA WA AMAN, BAADA YA ZANZIBAR KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF, LAKINI HOMA KALI NI KUJUA TIMU 12 ZA LIGI KUU ZITAPATIKANA VIPI?
Siku ya Alhamis Machi 16, 2017 itaendelea kukumbukwa na Wazanzibar baada ya ZFA
kuingizwa rasmi kuwa Mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF”
kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis
Ababa nchini Ethiopia.
Katika kura 54 za CAF, kura 51 zimekubali Zanzibar ipatiwe
uanachama wa kudumu wa Shirikisho hilo na nchi 3 zilikataa Zanzibar isipatiwe
ambazo ni Madagascar, Benin na Seychelles, hivyo Wazanzibar wala tusizichukie
nchi hizo kwani ni sehemu ya Demokrasia kuchaguwa ukipendacho.
Tangu viongozi wa ZFA pamoja na Waziri wa Habari Utalii
Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh Rashi Ali Juma warejee Visiwani Zanzibar wakitokea
huko Addis Ababa katika Mkutano huo mkuu walirejea na zawadi moja wapo ni
Bendera ya Shirikisho hilo la Soka Afrika “CAF”, Bendera ambazo tayari zimeshaanza
kupepea katika Viwanja viwili vikubwa hapa Zanzibar.
Katika Uwanja wa Amaan sehemu ya V.I.P nje kwenye bustani
ndogo Bendera hiyo ipo ina pepea halkadhalika na kule Kisiwani Pemba katika
uwanja wa Gombani.
![]() |
Bendera ya CAF ikipepea Amaan Zanzibar
Moja ya maagizo ya CAF ni kutaka msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ligi kuu soka ya Zanzibar iwe na jumla ya timu 12 kwa Zanzibar nzima ambapo kwasasa katika msimu huu wa mwaka 2016-2017 ina jumla ya timu 36 kwa kila kanda ina timu 18, yani Kanda ya Unguja 18 na Kanda ya Pemba 18, huku zikikushuka timu 12 kati ya hizo 36 kwa kila kanda kushuka timu sita (6).
Lakini Wadau wengi wa soka Visiwani Zanzibar wanahamu sana kujua mfumo gani utatumika kwaajili ya kupatikana timu 12 za ligi kuu soka ya Zanzibar kwa msimu ujao wa mwaka 2017-2018 ambapo Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA uliofanyika April 22 kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba umependekeza vilabu 28 vya ligi kuu ya Zanzibar msimu huu wakutane kwa pamoja baada ya kumalizika 8 bora na kupanga ni mfumo gani utumike ili zipatikane timu 12 za msimu ujao.
Timu hizo 28 ni zile ambazo zitanusurika kushuka daraja katika mkumbo wa awali ambapo hushuka timu 12 kwa kila kanda hushuka 6, yani Unguja 6 na Pemba pamoja na zile nne za Daraja la Kwanza zilizofanikiwa kuja juu ambazo ni mbili Unguja na mbili Pemba ndipo hapo zitakuwa Jumla ni timu 28.
Viongozi wa timu hizo 28 za Unguja na Pemba watakutana kwa pamoja baada ya kumalizika hatua ya 8 bora ambapo hapo ndipo patakapojulikanwa timu zipi zitacheza ligi kuu msimu ujao na mfumo gani utumike kupatikana kwa timu hizo 12.
Hivyo pengine huwenda timu ikafanikiwa kuwa bingwa au Mshindi wa Pili wa Zanzibar (Wawakilishi wa Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho) lakini akashindwa kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu ujao endapo akishindwa kuvuka katika mfumo huo ambao utakaotumika.
|
Comments
Post a Comment