BTMZ YATOA SIKU 30 VYAMA VYA MICHEZO KUFANYA UCHAGUZI
![]() |
Suleiman Pandu Kweleza- Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar |
BARAZA la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), limeviagiza vyama
vya michezo ambavyo havijafanya
uchaguzi kufanya hivyo ili kupata
viongozi kulingana na katiba zao na waziagize klabu zao kufanya uchaguzi ili
waongoze kwa demokrasia na kwa kufuata katiba.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa BTMZ, Khamis Ali Mzee
, iliyotolewa jana Afisini kwao Mwanakwerekwe, baraza hilo limetoa mwezi
mmoja (siku 30) kuanzia jana 16/5/2017 hadi 16/6/2017 ili kila chama na klabu kutekeleza maelekezo
hayo.
“Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar kupitia Afisi yetu ya
Mrajis wa Vyama vya Michezo na Vilabu tumegunduwa kuwa kuna vyama vya michezo
Taifa vimeshamaliza muda wao na bado vinaendelea kuwepo madarakani, sisi kama
Baraza hatukubaliani na baadhi ya Viongozi wa Vyama kujisahaulisha kufanya
uchaguzi, sasa tayari tushaweka wazi na kuna orodha ya vyama 5 vitaanza zoezi
hilo”. Alisema Mzee.
Nae Mrajisi wa vyama
vya michezo vya Zanzibar Suleiman Pandu Kweleza
amesisitiza vilabu kufuata kanuni na katiba ziilizowekwa kuanzia jana
hadi kufika tarehe 16-6- 2017
wawe wameshafanya uchaguzi na kupata viongozi wapya.
“Afisi yangu kuna vyama zaidi ya 33, kuna vingi sana
havijafanya uchaguzi, lakini kwa hatua ya kwanza tunaanza na vyama 5 ambavyo
hima hima wanatakiwa wafanye uchaguzi wao na ikifika tarehe 16-6- 2017 wawe
wameshafikia pazuri kwenye uchaguzi”. Alisema Kweleza.
Vyama vitano (5) ambavyo vinaharakishwa kufanya uchaguzi ni Chama
cha Basketball Zanzibar (BAZA), Chama cha Baskeli Zanzibar (CHABAZA), Chama cha
Mpira wa Netball Zanzibar (CHANEZA), Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar yani Hand
ball na Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar yani Table Tennis.
Comments
Post a Comment