CHAMA CHA SQUACH CHAPATA UONGOZI MPYA

Chama cha Mpira wa Ukuta Zanzibar “Zanzibar Squash Racket Association (ZSRA)” kimepata viongozi wapya watakaongoza kwa kipindi cha miaka minne ijayo baada ya leo asubuhi Jumamosi Mei 6, 2017 kufanyika Uchaguzi katika Ukumbi wa Squach uliopo Polisi Ziwani.

Katibu wa Kamati ya Uchaguzi Yussuf Mohd Ali amewatangaza washindi kwa nafasi sita zilizogambaniwa katika Uchaguzi huo ambapo kwa nafasi zote wagombea walikuwa mmoja mmoja na wapiga kura walikuwa 13 hivyo kura zilipigwa kwa ndio na hapana.

Amemtangaza Abuza Salim kuwa Mwenyekiti mpya kwenye chama hicho baada ya kura 13 zote kumkubali, nafasi ya Makamo Mwenyekiti akashinda Omar Yussuf Omar baada ya kupata kura 10 huku kura 1 ilimkataa na kura 2 ziliharibika, nafasi ya katibu amejitokeza Mohd Hamza Ali  kashinda kwa kura 10, kura 1 ikiharibika na kura 2 zilimkataa, huku naibu katibu ameshinda Nassor Salum Mohammed baada ya kura 12 kumkubali na 1 kumkataa.

Wakati huo huo Mwanamama pekee katika uchaguzi huyo Fatma Saleh Amani ameshinda nafasi ya mshika fedha baada ya kushinda kura 11 huku kura 1 ikimkataa na 1 kuharibika, wakati Iddi Khamis Yussuf nae ameshinda nafasi ya Mshika Fedha Msaidizi baada ya kupata kura 11 na kura 1 ilimkataa huku 1 iliharibika.

Kamati ya Uchaguzi iliyosimamia uchaguzi huo ina Wajumbe 7 wakiongozwa na Mwenyekiti Abdallah Juma na Katibu Yussuf Mohd Ali “Kareka” huku wajumbe wakiwa Juma Mussa Rashid, Omar Makungu Omar, Mwanaidi Abdallah Makame, Zuhura Mohd Ali na Hadia Yahya Khamis.


Viongozi hao wataongoza kwa muda wa miaka 4 ijayo ndipo utafanyika mwengine kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE