HATMA YA MALINDI, KIPANGA NA KILIMANI CITY NANI ATAUNGANA NA TIMU 5 KUSHUKA DARAJA LEO HUWENDA TUKAPATA KUJUA
![]() |
Kikosi cha Kilimani City |
Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja leo itaendelea tena
kwa kupigwa michezo 3 katika viwanja viwili tofauti ambapo michezo hiyo
inahusisha timu zote ambazo zipo hati hati kuungana na timu 5 kushuka daraja.
Timu 5 ambazo tayari zishajihakikishia kushuka daraja ni
Kimbunga, Chaka Stars, Miembeni, Kijichi na Mundu ambapo wanaisubiri timu moja
ili ziwe 6 kuungana kushuka daraja na homa kubwa ipo kwa vilabu vitatu ambavyo
ni Malindi, Kipanga na Kilimani City na mmoja kati ya hao wataungana na vilabu
vyengine vitano ambavyo tayari vishajihakikishia kushuka daraja.
![]() |
Saleh Machupa kocha wa Malindi |
MALINDI
Malindi imebakisha michezo 2 baada ya kucheza michezo 32 hadi
sasa na kati ya michezo iliyosalia upande wao watacheza leo Jumatano 3/5 dhidi
ya KMKM saa 8:00 Amaan na mwengine
watamalizana na Taifa ya Jang’ombe ambao watacheza Jumamosi 06-05-2017 saa10:00
Amaan.
Malindi ipo nafasi ya 13 wana alama 39 katika michezo 32
waliyocheza wameshinda 11 sare 6 na kupoteza 15.
|
![]() |
Kikosi cha Kipanga |
KIPANGA
Timu hii inamilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) ambapo wamebakiwa na michezo miwili kati yao na KVZ utakaochezwa leo Jumatano 3/5/2017 saa 10:00 Amaan, na mchezo wao wa mwisho watamalizana
na KMKM Jumapili ya 07-05-2017 saa 1:00 USIKU Aman.
Katika Msimamo wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama 41 kati ya
michezo 32 waliyocheza wameshinda 12, sare 5 na wamefungwa 15.
KILIMANI CITY
Kilimani City wenyewe wanajita watoto wa Mjini wamebakiwa na
michezo 2 , mmoja watacheza leo Jumatano 03/5/2017 dhidi ya Jang’ombe Boys saa
10:00 jioni katika uwanja wa Fuoni, na wa mwisho watamalizana na Chuoni Tarehe
05-05-2017 saa 1:00 za usiku Amaan.
Katika msimamo wapo nafasi ya 11 katika michezo 32
waliyocheza wameshinda 13, sare 4 na kupoteza 15.
Kati ya Malindi, Kipanga na Kilimani City nani ataungana na Kimbunga,
Chaka Stars, Miembeni, Kijichi na Mundu kushuka Daraja?, jawabu lake huenda
tukaanza kulipata jioni ya leo baada ya kumalizika kwa michezo yote hiyo
mitatu.
Comments
Post a Comment