HIYO NDO NEMBO MPYA YA ZFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF
Chama cha soka Visiwani Zanzibar kimefanya marekebisho ya
nembo yao na sasa watatumia nembo hiyo (Pichani) katika shughuli zao zote za
Chama hicho.
Siku ya Alhamis Machi 16, 2017 itaendelea kukumbukwa na Wazanzibar baada ya ZFA
kuingizwa rasmi kuwa Mwanachama wa 55 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF”
kufuatia Kikao cha 39 cha Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo kilichofanyika Addis
Ababa nchini Ethiopia.
Katika kura 54 za CAF, kura 51 zimekubali Zanzibar ipatiwe
uanachama wa kudumu wa Shirikisho hilo na nchi 3 zilikataa Zanzibar isipatiwe
ambazo ni Madagascar, Benin na Seychelles.
Tangu viongozi wa ZFA pamoja na Waziri wa Habari Utalii
Utamaduni na Michezo Zanzibar Rashid Ali Juma warejee Visiwani Zanzibar wakitokea
huko Addis Ababa katika mkutano huo, ZFA wakaanza kazi ya kuirekebisha nembo
yao.
![]() |
Nembo ya ZFA ya Zamani |
Comments
Post a Comment