ILI KIPANGA ASISHUKE DARAJA LAZIMA ASIFUNGWE KESHO NA KMKM BAADA YA LEO MALINDI KUIFUNGA TAIFA

Timu ya Malindi kushuka au kutoshuka daraja hatma yao ipo mikononi mwa KMKM kesho watakapocheza na Kipanga majira ya saa10:00 za jioni kwenye uwanja wa Aman.

Leo klabu ya Malindi imepata alama tatu muhimu na kuzidi kuwatia tumbo joto Kipanga baada ya kuwafunga Taifa ya Jang’ombe bao 1-0 mchezo uliopigwa saa 10 za jioni katika uwanja wa Amaan.

Bao pekee la Malindi limefungwa na Kassim Khalfan dakika ya 68 na kusubiri mchezo wa kesho ambapo Malindi anaiombea dua Kipanga ifungwe na KMKM ili wao wanusurike kushuka daraja.

Malindi baada ya kushinda leo amefikisha alama 42 ambapo Kipanga ana alama 41 na kesho akifungwa Kipanga atashuka wao na endapo akitoa sare Kipanga atabakia kwa kufikisha alama sawa na Malindi 42 lakini Kipanga atakuwa ana faida ya mabao baada ya kuwa na akiba ya mabao 4 huku wenzao Malindi bado wana deni la mabao 7.


Kikosi cha Kipanga
Mchezo mwengine uliopigwa leo mapema saa 8 za mchana Mafunzo wakaichapa Jang’ombe Boys bao 1-0, bao lilofungwa na Rashid Abdallah katika dakika ya 33.

Michezo mengine ya mwisho kesho kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja utapigwa majira ya saa 8:00 za mchana kati KVZ dhidi ya Kimbunga katika Uwanja wa Amaan, na saa 10:00 za jioni Fuoni watasukumana kati ya Kijichi dhidi ya Chwaka Stars.

Kesho ligi hiyo itamaliza rasmi kwa kila timu kukamilisha idadi ya michezo 34 ambapo timu 4 za Unguja zilizofuzu 8 bora tayari zishajulikana ambazo ni JKU, Jang’ombe Boys, Zimamoto na Taifa ya Jang’ombe lakini kwa upande wa timu 6 za kushuka daraja 5 kati ya hizo zishajulikana ambazo ni Kimbunga, Chaka Stars, Miembeni, Kijichi na Mundu, hivyo kati ya Malindi na Kipanga nani ataungana na kushuka Daraja na hao?, jawabu lake tutalipata kesho katika mchezo wa Kipanga dhidi ya KMKM.

Comments

Popular posts from this blog

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

ZANZIBAR KARIBU WATAPATA UANACHAMA WA FIFA BAADA YA KUWA MWANACHAMA WA 55 WA CAF

JKU ACADEMY HAO WATANGULIA KWENDA ARUSHA KATIKA MASHINDANO YA ROLLING STONE