JE UNAJUA KUWA TIMU 12 ZILIZOSHUKA LIGI KUU YA ZENJ ZOTE ZA URAIANI?
![]() |
Kikosi cha Miembeni |
Ligi kuu soka ya Zanzibar msimu huu wa mwaka 2016-2017 ulikuwa una jumla ya timu 36 kwa kila kanda timu 18, yani kanda ya Unguja 18 na Pemba 18.
Katika vilabu hivyo 36, klabu za Uraiani vilikuwa 28 huku timu za Vikosi zilikuwa 8.
Timu hizo 8 za Vikosi ni JKU, Zimamoto, KMKM, Mafunzo, KVZ ambavyo ni Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) , vyengine ni Polisi, Kipanga na Hardrock (JWTZ) vyote vikitoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Timu 12 zilizoshuka daraja kutoka ligi kuu hadi Daraja la Kwanza Taifa kutoka Unguja ni Malindi, Kijichi, Mundu, Miembeni, Chwaka stars na Kimbunga wakati zile za Pemba ni Maji maji, Sharp Victor, Aljazira, Danger Boys, African Kivumbi, na Madungu.
Uwepo wa Vilabu vingi vya Mitaani hasa vinavyotoka kwenye mitaa husika kama vile Chwaka, Miembeni, Malindi, Madungu na Kijichi vilitegemewa vitafanya vizuri katika ligi hiyo kwa vile vimebeba jina la mtaa husika lakini mwisho wa ligi vimeteremka daraja.
Na: Mossi Abdallah, Zanzibar.
Na: Mossi Abdallah, Zanzibar.
![]() |
Kikosi cha Chwaka Stars |
Comments
Post a Comment