JIMBO LA KIKWAJUNI LAUNGANA NA MALINDI NA KWAHANI NUSU FAINALI
Ligi ya Majimbo imeendelea tena jioni ya leo Jumamosi katika
uwanja wa Polisi Ziwani huku tukishuhudia Jimbo la Kikwajuni kutinga hatua ya
nusu baada ya kulitoa jimbo la Mfenesini kwa penalti 5-4 kufuatia dakika 90
kumalizika kwa sare ya 0-0.
Kikwajuni wataungana nusu fainali na Jimbo la Malindi na Kwahani wakimsubiri mshindi wa robo fainali ya mwisho itakayopigwa kesho saa 10 katika Uwanja wa Polisi Ziwani kati ya Timu ya Afisi kuu ya CCM dhidi ya timu ya Kaskazini.
Bingwa wa Mashindano hayo ya Majimbo atazawadiwa Gari aina ya Carry.
|
Comments
Post a Comment