KAMPUNI YA SANSI YAIPIGA TAFU TIMU YA GULIONI KWA KUIDHAMINI ASILIMIA 60
![]() |
Suhail Suleiman Mkurugenzi wa Kampuni ya SANSI |
Akizungumzia lengo la kuidhamini timu hiyo Suhail Ibrahim ambae
ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo amesema kikubwa kilichomvutia mpaka kampuni yake
ikaidhamini Gulioni kwakuwa timu hiyo inamvuto mkubwa sana na hamasa ya
Mashabiki wake.
“Kampuni yangu imevutiwa na hamasa ya Mashabiki wa Gulioni,
ndio maana nikaamua kuidhamini timu hii, udhamini wetu ni kwa asilimia 60 timu
itaidhamini na huko mbele ikiwa mambo yatakwenda vizuri tutazidi kuidhamini kwa
asilimia kubwa zaidi”. Alisema Suhail.
Nae Ahmed Khamis ambae ni Rais wa Gulioni FC ameishukuru sana Kampuni hiyo kwa udhamini wao huku akiwaahidi Mashabiki wa Gulioni watazidi kufanya vizuri katika hatua ya 4 bora baada ya udhamini huo.
“Tunaishukuru Kampuni ya SANSI kwa udhamini wao, kwani kuna vilabu vingi kaviacha kaja kwetu Gulioni, tunawashukuru sana na pia tunawakaribisha na tutafanya kazi vizuri ili lengo letu litimie, naamini katika hatua ya 4 bora inayoendelea tutazidi kuwa bora baada ya udhamini huu”. Alisema Ahmed.
|
Comments
Post a Comment