KIKOSI CHA UMISSETA KANDA YA UNGUJA CHAWEKWA HADHARANI, JUNE 3 WATAENDA MWANZA
Kocha msaidizi wa timu ya soka Kanda ya Unguja Abdul wahab
Dau “Mwalimu Dau” ametangaza kikosi kipya wachezaji 22 cha timu hiyo ambacho
kinatarajiwa kwenda Butimba Jijini Mwanza katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa
Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)yanayotarajiwa kuanza June 6, 2017.
Wachezaji hao 22 watachujwa 4 na kubakia 18 ambao
watakaokwenda katika Mashindano, mchujo wa mwisho unatarajiwa kufanywa siku
chache kabla ya safari.
Kikosi hicho cha wachezaji 22 wa kanda ya Unguja Walinda
mlango ni:-
Aley Ali Suleiman (Ubago) na Abass Wadi (Philter)
Wachezaji wengine ni Ahmed Mohd Shaaban (Nyuki), Amani Ali
Suleiman (Kiembe Samaki), Ali Mohd Seif (Tumekuja), Ali Issa (Lumumba), Jamali
Ali Jaku (Kinuni), Elias Suleiman (K-pura) na Abdurahman Seif Bausi (Glorious).
Wengine ni Ibrahim Faraj (Lumumba), Faki Kombo (JKU Mtoni),
Haji Suleiman (JKU Mtoni), Mundhir Abdallah (JKU Mtoni), Ali Hassan (Bububu),
Abdul aziz Ameir Khatib (Arahman), Walid Abdi (Mwera), Mansour Mohd (Mtoni),
Abubakar Khamis (Bububu), Abdulatif Mzee (Philter), Habibu Ali (Nyerere),
Ibrahim Abdallah Hamad (Arahman) na Yakoub Kiparo (Langoni).
Mashindano ya UMISSETA yanayotarajiwa kuanza June 6, 2017
huko Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu Zanzibar
itashiriki kanda mbili tofauti, yani Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.
Comments
Post a Comment