KIKOSI KIPYA CHA KOMBAIN YA MJINI ROLLING STONE CHAKUTANA LEO
Kikosi cha wachezaji 37 cha Kombain Wilaya ya Mjini ambacho
kinatarajiwa kwenda Arusha katika Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki ya
Rolling Stone kimekutana asubuhi ya leo na viongozi wa timu yao inayoongozwa na
Kocha Mkuu Mohammed Seif “King” .
Wachezaji hao
wamekutana katika Ukumbi wa Uwanja wa Amaan ambapo wameenda kujuana na kisha
kupanga mikakati yao ya kuanza mazoezi ambapo wakitarajiwa kufanya mazoezi kila
siku ya Jumamosi na Jumapili asubuhi katika Uwanja wa Amaan.
Benchi la
Ufundi la timu hiyo linaongozwa na Kocha Mkuu Mohammed Seif “King”, Kocha
Msaidizi Ramadhan Abdul rahman “Madundo”, Meneja wa Timu Ali Othman “Kibichwa”,
Kocha wa Makipa Salum Ali “Chulas” na Mtunza vifaa Nassir Kheir.
Wachezaji 37
wa awali waliotangazwa wiki iliyopita ni:-
Walinda
Mlango ni Rajab Farouk Festo (Real Kids), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na
Makame Mkadar Koyo (Huru).
Wachezaji wa
ndani ni Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Mahad Hassan
Bai (Kijangwani), Yahya Silver (Muembe ladu), Shaaban Pandu (Villa United),
Saleh Khatib (Kijangwani), Idrissa Makame (Villa FC), Ramadhan Simba (Calypso),
Khatib Kombo (Schalke 04), Othman Jumbe (Black Sailors), Ali Hassan (Uhamiaji),
Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe
Boys), Nassir Ramadhan (Muembe Makumbi) na Mohd Ridhaa (Villa United).
Wengine ni
Mussa Shaaban (Zimamoto), Ismail Kassim (Huru), Seif Said (KVZ), Abdillah
Suleiman (King Boys), Haji Suleiman (JKU), Mohd Jailan (Chrisc), Makame Maoud
(Schalke 04), Fahad Mussa (Mapembeani), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma
(KMKM), Suleiman Dorado (Uhamiaji), Said Salum (Real Kids), Mohd Haji
(Jang’ombe Boys), Abrahman Juma (ZAFSA), Abdul-hamid Juma (ZAFSA), Khatib Ameir
(Real Kids), Yussuf Mohd (Muembe Beni) na Ibrahim Chafu (Villa FC).
Comments
Post a Comment