KILIMANI CITY YAPANIA KUMLETA KOCHA KUTOKA MISRI, MAZUNGUMZO YAO YAMEFIKIA PAZURI
![]() |
Mohammed Mbaraka "Mebo" |
Baada ya kunusurika kushuka daraja kwenye mkumbo wa awali
ligi kuu soka ya Zanzibar, klabu ya Kilimani city imepania kumleta kocha kutoka
nchini Misri ambae ni Mohammed Mbaraka “Mebo”na mazungumzo yamefikia patamu
kati yao.
Akizungumza na kisanduzenj.blogspot.com Rais wa Kilimani City
Khamis Shaali amesema wameshaanza mazungumzo na kocha huyo na tayari wasifu
wake ameshawatumia (CV) na uongozi wao City wameridhika na sifa za mwalimu
huyo.
Amesema wanatarajia kumleta kocha Mebo ambae ana leseni B ya
Shirikisho la Soka Afrika na msimu mpya ukianza kocha huyo ataonekana katika
soka la Zanzibar akiwa na klabu ya Kilimani city.
“Mipango yetu na kocha Mohammed Mubarak yanakwenda vizuri na
msimu ujao tutakuwa nae ligi ikianza kocha huyu ni kutoka Misri, na tayari
kashatuma CV zake kama unavyoziona hapa, anasifa nyingi sana nzuri na
tumeipenda CV yake”, Alisema Shaali.
Katika ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja Kilimani
City imenusurika kushuka daraja katika mkumbo wa awali baada ya kumaliza ikiwa
nafasi ya 11 wakiwa na alama 47 kwa michezo 34 ya ligi hiyo.
City ni miongoni mwa timu 28 za Unguja na Pemba ambazo
zitapigania katika kinyanganyiro cha kutafuta timu 12 ambazo zitacheza ligi kuu
msimu ujao, msimu ambao zinatakiwa timu 12 tu pekee, baada ya kumalizika hatua
ya 8 bora, hapo ndipo patakapojulikanwa timu zipi zitacheza ligi kuu msimu huo
na mfumo gani utumike kupatikana kwa timu hizo 12 baada ya kukaa kwa pamoja
viongozi wa timu hizo 28 na kupanga mfumo gani watumie ili wazipate timu hizo 12.
Comments
Post a Comment