KIPANGA YAISHUSHA DARAJA MALINDI
Leo rasmi timu ya Malindi imeungana na Kimbunga, Chwaka Stars,
Miembeni, Kijichi na Mundu kushuka daraja kutoka ligi kuu hadi ligi daraja la
Kwanza baada ya jioni ya leo Kipanga kutoka sare ya 2-2 dhidi ya KMKM katika mchezo
wa mwisho wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliopigwa katika uwanja
wa Amaan.
Kwa matokeo hayo Kipanga imemaliza ligi hiyo salama ikiwa na
alama sawa na timu ya Malindi iliyoshuka daraja wote wana point 42 lakini
Kipanga ana faida ya mabao baada ya kuwa na akiba ya mabao 4 huku wenzao
Malindi wana deni la mabao 7 na kusababisha kushuka daraja.
Mchezo mwengine leo KVZ wakaitandika Kimbunga mabao 6-1
uliosukumwa saa 8 za mchana katika Uwanja wa Amaan huku Kijichi wakaichapa Chwaka
Stars 1-0 mchezo uliopigwa majira ya saa 10 za jioni Fuoni .
Comments
Post a Comment