LUMUMBA YAPIGWA NA UMISSETA MBELE YA MKURUGENZI WA MICHEZO WIZARA YA ELIMU

Kikosi cha UMISSETA Unguja

Katika kujiweka sawa na Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) timu ya Kanda ya Unguja imecheza mchezo wa kirafiki na timu ya Shule ya Lumumba katika Uwanja wa Amaan asubuhi ambapo timu ya UMISSETA ya Unguja ikafanikiwa kuibuka na Ushindi wa Mabao 3-1.

Mabao ya Kombain ya UMISSETA yamefungwa na Ali Mohd dakika ya 4 na 50, na jengine likifungwa na Iliyasa Suleiman dakika ya 26.


Bao pekee la Lumumba limefungwa na Ali Assaa dakika ya 32.
Kikosi cha Shule ya Lumumba
Hassan Tawakal Khairallah Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar akiwasalimia timu ya UMISSETA Kanda ya Unguja.


Mashindano ya UMISSETA yanatarajiwa kuanza June 6, 2017 huko Butimba Mkoani Mwanza ambapo Zanzibar mwaka huu zitatoa kanda mbili tofauti, Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba.

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS