MADUNDO ATANGAZA KIKOSI KIPYA CHA WILAYA YA MJINI, WALOCHUKUA UBINGWA WOTE WAPIGWA CHINI KASORO MMOJA TU
![]() |
Ramadhan Abdurahman "Madundo" |
Mbali na kutangaza
kikosi cha wachezaji 37, Madundo ametaja vipaombele vyake kwenye timu hiyo
ambavyo amezingatia katika kuteua majina hayo.
Amesema kitu
pekee ambacho wameangalia ni uwezo wa mchezaji na nidhamu ndani na nje ya
uwanja ili kuweza kujenga timu imara ambayo itakuwa na uwezo wa kupambana kwa
kuwawakilisha Zanzibar katika Mashindano hayo.
Aidha Madundo
amesema katika Kikosi hicho wameamua kuwaacha wachezaji wote waliotwaa Ubingwa msimu
ulopita Jijini Arusha na kuwemo mmoja tu ambae ni Abdurahman Juma “Baby” wa
KMKM huku sababu kuu akisema kuwa umri wao umekuwa mkubwa ndio mana
wamelazimika kutowajumuisha.
Kikosi kipya
cha Kombain ya Mjini ni:-
Walinda Mlango
ni Rajab Farouk Festo (Real Kids), Peter Dotto Mashauri (Schalke 04) na Makame
Mkadar Koyo (Huru).
Wachezaji wa
ndani ni Hassan Chalii (Kipanga), Abdul-halim Ameir (King Boys), Mahad Hassan
Bai (Kijangwani), Yahya Silver (Muembe ladu), Shaaban Pandu (Villa United),
Saleh Khatib (Kijangwani), Idrissa Makame (Villa FC), Ramadhan Simba (Calypso),
Khatib Kombo (Schalke 04), Othman Jumbe (Black Sailors), Ali Hassan (Uhamiaji),
Fahmi Salum (Mlandege), Salum Omar (Villa United), Yakoub Omar (Jang’ombe
Boys), Nassir Ramadhan (Muembe Makumbi) na Mohd Ridhaa (Villa United).
Wengine ni
Mussa Shaaban (Zimamoto), Ismail Kassim (Huru), Seif Said (KVZ), Abdillah
Suleiman (King Boys), Haji Suleiman (JKU), Mohd Jailan (Chrisc), Makame Maoud (Schalke
04), Fahad Mussa (Mapembeani), Mohd Mussa (Mapembeani), Abrahman Juma (KMKM), Suleiman
Dorado (Uhamiaji), Said Salum (Real Kids), Mohd Haji (Jang’ombe Boys), Abrahman
Juma (ZAFSA), Abdul-hamid Juma (ZAFSA), Khatib Ameir (Real Kids), Yussuf Mohd
(Muembe Beni) na Ibrahim Chafu (Villa FC).
Jumapili ya
Mei 7, 2017 benchi la Ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Kocha Mohammed Seif “King”
litakutana na wachezaji wote
walioteuliwa kuanzia saa 4:00 za asubuhi kwenye Afisi ya ZFA Wilaya ya Mjini,
Aman ili kuzungumza nao na kupanga utaratibu wa kuanza mazoezi.
Comments
Post a Comment