MAJI MAJI YASHUSHWA KUTOKA LIGI KUU HADI DARAJA LA KWANZA
![]() |
Ali Mohammed Makamo Urais wa ZFA PEMBA |
ZFA Taifa Pemba imeiteremsha daraja timu ya Maji Maji kutoka
ligi kuu ya Zanzibar, hadi daraja la kwanza Taifa msimu wa 2017/2018, pamoja na
kuitoza faini ya shilingi Milioni 1,200,000/= kwa makosa mawili tafauti.
Kosa la kwanza kwa Timu hiyo katika mchezo wake na Shaba wa
Aprili 28 mwaka huu, timu ya Maji Maji ilifika Uwanjani na wachezaji nane tu na
kupekea baadhi ya wachezaji kuanguka uwanjani na kushindwa kuendelea
na mchezo huo.
Kaimu Msaidizi Katibu Mkuu ZFA Taifa Khamis Hamad Juma, alisema
baada ya hali hiyo mwamuzi wa mchezo huo alilazimika kulivunja pambano hilo
dakika ya 44, huku Shaba ikiwa inaongoza kwa goli 1-0.
“Kutokana na hali ilivyokuwa uwanjani baada ya wachezaji
watatu kuumia, wakabakia wachezaji watano mwamuzi hakuweza kuendelea na mchezo
na kulivuanja pambano”. Alisema.
Alisema kwa mujibu wa kanuni za kuendeshea mashindano ya
Mpira wa Miguu Zanzibar, Kifungu namba 21 (a)(i) timu ya Maji Maji imepoteza mchezo
huo na shaba kuwepwa ushindi, pamoja na kuteremsha daraja la
kwanza Taifa n kwa msimu 2017/2018 na kutozwa faini ya laki
600,000/= faini ambayo inatakiw akulipwa Mei 30 mwaka huu.
Khamis alisema kosa la pili kwa timu hiyo katika mchezo wake
na Jamhuri wa Aprili 26 mwaka huu katika uwanja wa FFU Finya, ulishindwa kumalizika
kwa wakati baada ya wachezaji Abrahman Haji Othaman alikuwa
na jezi No. 30 c/No. 020, Bakar Said Ginyari Jezi No. 11C/No.
013, Branka Ali Yassin jezi NO. 9 C/No. 024 na Ibrahim Said Juma jezi No.17.
Wachezaji hao walidaiwa kumpiga mwamuzi Seif Kesi na
kumsababishia maumivu makali pamoja na kupoteza vifaa vyake alivyokuwa akitumia
kwa ajili ya maamuzi anapokuwa kiwanjani na kushindwa kabisa kuendelea
kuchezesha mchezo.
Alisema kwa mujibu wa kanuni ya mashindano kifungu namba 26
C(1), Maji Maji imepoteza mchezo huo na kupewa timu ya Jamhuri, huku wachezaji hao
wane wakifungiwa kucheza ligi kwa msimu miwili 201/2018 na
2018/2019 na kutozwa faini ya shilingi laki 600,000/=
inayotakiwa kulipwa Juni 26 mwaka huu.
Kwa matokeo hayo Timu ya Maji Maji, MADUNGU, African
Kivuymbi, Aljazira, Danger Boys na Sharp Victor zimeshuka daraja kutoka ligi
kuu ya Zanzibar kwa msimu wa 2016/2017.
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
Comments
Post a Comment